Kwingineko

Suarez kama Messi Inter Miami

NYOTA wa Uruguay Luis Suarez anatarajiwa kujiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani kama walivyofanya Lione Messi na Sergio Busquets.

Tayari Messi amethibitisha kuwa atajiunga na Inter Miami majira haya ya joto ambako ataungana rafiki yake wa karibu Sergio Busquets.

Messi atasajiliwa timu hiyo ya ligi kuu Marekani(MLS) akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Paris Saint-Germain hivyo hivyo kwa Busquets aliyeondoka Barcelona msimu wa 2022/23.

Suarez amekuwa akiichezea timu ya Gremio ya Brazil tangu msimu uliopita baada ya kuondoka timu ya nyumbani kwao Uruguay ya Nacional.

Mkataba wa Suarez mwenye umri wa miaka 26 katika klabu ya Gremio unafikia ukingoni mwaka 2024 lakini ana kipengele cha kuachiwa ambacho yeye na Miami wamekiboresha na uhamisho wake utathibitishwa hivi karibuni.

Wachezaji hao watatu walitumikia Barcelona miaka sita kwa mafanikio na inaaminika Messi amehusika kwa kiasi kikubwa kusaidia Suarez na Busquets kuhamia Inter Miami.

Related Articles

Back to top button