Ligi Ya WanawakeNyumbani
Stumai mchezaji bora Ligi Wanawake mwezi Mei

Mchezaji Stumai Abdallah wa klabu ya JKT Queens amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
JKT Queens ndio bingwa mpya wa ligi hiyo msimu wa 2022/2023 baada ya kukusanya pointi 46 kwa michezo 18 bila kufungwa.
Timu hiyo itashiriki michuano ya Afrika kwa wanawake.