Kwingineko

Steve atangaza kusimama na Nicole

MWIGIZAJI wa vichekesho Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ametangaza kusimama na mwigizaji Joyce Mbaga ‘Nicole’ ili kumsaidia kupata dhamana.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Steve Nyerere ameweka ujumbe na kusema hakuna sababu ya kuangalia makosa yake kwa kuwa hakuna aliyekamilika.

Nicole yuko chini ya ulinzi na ameshtakiwa kwa makosa ya kuendesha genge la uhalifu na kupokea pesa shilingi milioni 185.5 za Tanzania kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Steve amesema hakuna haja ya kuangalia amefanya nini, bali kuangalia uwezekano wa kumsaidia kupata dhamana yake kwani anapitia kipindi kibaya sana ambacho anahitaji faraja.

“Tusimame kumuombea dhamana tunajua na kutambua sheria na kuheshimu sheria kwenye Taifa letu,
“Niombe sio muda wa kuliangalia kosa ni muda wa kulitibu kosa nani mkamilifu hapa Duniani,

“Mimi Binafsi kama Steven Mengele nipo tayari kumsaidia kutoka ndani kwa kufuata taratibu zote na akipata dhamana basi atambue kulipa kial jasho la mchangiaji kurudishiwa na maisha kuendelea hakuna mwanadamu ambaye mkamilifu hapa duniani,”amesema.

Related Articles

Back to top button