Ligi Daraja La Kwanza
Stephen Sey atua Dodoma Jiji

Mshambuliaji wa zamani wa Singida United na Namungo Stephen Sey amejiunga na Dodoma Jiji.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ghana amejiunga na Dodoma Jiji kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ambapo timu zinaendelea kuimarisha vikosi vyao.
Mchezaji huyo alikuwa huru baada ya kutokuwa na timu kwa zaidi ya miezi sita kufuatia kuvunja mkataba na klabu ya amani ya El Sharkia ya Misri.
Dodoma Jiji itarejea kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara Januari 14 kwa mchezo wa ugegeni dhidi ya Geita Gold.




