EPL
Spurs yapata kocha wa mataji

Ange Postecoglou ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Tottenham kwa mkataba miaka minne hadi Juni 2027.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amesema: “Ange huleta mawazo chanya na mtindo wa kucheza wa haraka na wa kushambulia.”
Kocha huyo anajiunga na Spurs kuchukua nafasi ya Antonio Conte, aliyetimuliwa mwezi Machi kutokana na matokeo mabovu.
Postecoglou amejiunga na timu hiyo yenye maskani yake London akitokea Celtic ya Scotland.




