Habari Mpya

Southgate ajiuluzu England

LONDON: KOCHA Gareth Southgate wa England amejiuzulu kuifundisha timu baada ya kukosa ubingwa wa Euro 2024 katika mchezo wa fainali kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Hispania juzi.

“Nikijuvunia kuwa Mwingereza, imekuwa heshima ya maisha yangu kucheza na kuifundisha England kwa miaka hii.”

“Hii ina maana kubwa sana kwangu, nimetoa kila kitu.” Lakini ni muda wa mabadiliko na ukurasa mpya naachia ngazi kama meneja, nimefanya maamuzi hayo.”amesema Southgate.

Southgate ,53, alikosa ubingwa wa Euro miaka mitatu iliyopita uwanja wa Wembley dhidi ya Italia, lakini pia dhidi ya Hispania juzi.

Related Articles

Back to top button