Nyumbani

Somoe Ng’itu na Zena Chande waula TWFA

KILIMANJARO:WAANDISHI wa Habari wakongwe Somoe Ng’itu na Zena Chande wamechaguliwa kuongoza  Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mkoani Kilimanjaro leo.

Somoe ambaye ni mwandishi wa gazeti la Nipashe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TWFA na Zena ambaye ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la HabariLEO amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Somoe alipata kura 37 na mpinzani wake Amina Karuma alipata kura 14 huku Zena akipata kura 34 na wapinzani Fatuma Seleman kura tisa pamoja na Veronica Samo aliyepata kura nane.

Katika nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji Irene Ishengoma, Ndinagwe Sungura walipita bila kupingwa baada ya Mwanaheri Kalolo kujitoa siku ya uchaguzi.

Baada ya Somoe kutangazwa na kuapishwa, alimteua Beatrice Mgaya kuwa Makamu Mwenyekiti na Hamisa Katambi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo Benjamin Kalume baada ya kutangaza matokeo aliwataka viongozi hao wakafanye kazi kwa ushirikiano na kuvunja kambi kwani uchaguzi umekwisha.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button