Simba inatoa somo Kimataifa

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imefanikisha kampeni yao ya kuongoza kundi kwa kukusanya pointi 13 baada ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya CS Constantine katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Bao la kuongoza la Simba limefungwa na Denis Kibu dakika ya 61, akimalizia pasi ya Mpanzu. Dakika ya 79 Lionel Ateba ameipatia bao la pili, wekundu wa msimbazi baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Shomari Kapombe.
Ushindi huo umeishusha CS Constantine hadi nafasi ya pili akiwa na alama 12 wakati timu zote zimefuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo.
Kipindi cha kwanza kimetamatika Simba 0-0 CS Constantine, timu zote zilicheza vizuri kila mtu alipata nafasi ya kufika katika lango la mwenzake.
Ndani ya dakika 45 ya kipindi cha kwanza Simba walifanikiwa kupiga mashuti 6, moja limelenga lango la CS Constantine, Shambulizi la Leonel Ateba dakika ya 26 akiwa na kipa Zakaria Bouhalfaya kuudaka mpira.
Wakati CS Constantine walipiga shuti moja ambalo limelenga lango la mpinzani wake 0-0dakika ya 28 kupitia mchezaji wake Ibrahim Dib alipiga shuti lakini kipa wa Simba, Moussa Camara amekuwa makini na kudaka mpira.
Muamuzi wa mchezo Celso Alvacao kutoka Msumbiji amewapa kadi ya njano mchezaji wa Simba, kibu Denis dakika ya 8 baaada ya kumfanyia madhambi nyota wa CS Constantine, Houari Baouchaa alipewa kadi ya njano dakika ya 10 akimchezea rafu Shomari Kapombe
Baada ya kutamatika kwa dakika 90 ya mchezo huo kipa wa CS Constantine, Houari Baouchaa amewafuata nyota wawili wa Simba, Fabrice Ngoma na Ateba na kuwaomba jezi za klabu hiyo ya mitaa ya Msimbazi.