Filamu

Shubhangi atoa machozi akikumbuka kifo cha mume wake

INDIA: NYOTA wa filamu ya ‘Bhabhi Ji Ghar Par Hain’, Shubhangi Atre, bado anasumbuliwa na kumbukumbu za kifo cha mume wake, Piyush Poorey, aliyefariki Aprili mwaka huu 2025.

Muigizaji huyo amesema kwamba madaktari walikuwa wamewaidhinisha kuhusu matokeo yanayoweza kutokea ikiwa mume wake huyo Piyush hangebadilisha mtindo wake wa maisha na kushinda uraibu wake.

Piyush Poorey, alifariki kwa ugonjwa wa ini. Muigizaji huyo katika video ya mahojiano hayo anaonekana akipata hisia wakati akizungumza kuhusu Piyush.

Amesema: “Nadhani ni kwa sababu ya uraibu. Madaktari hawana shida, nitasema tu kwamba haikuwa bahati. Madaktari walikuwa wamemwambia hii inaweza kutokea mapema kwamba kama angebadilisha maisha yake,’ lakini sikujua kama angefariki mapema hivyo”.

Ameongeza: “Nataka kumkumbuka kwa mambo yote mazuri. Nilimpenda, na huenda siwezi kamwe kusahau kuhusu hilo.”

Wanandoa hao walifunga pingu za maisha huko Indore Shubhangi na Piyush walifunga ndoa mwaka wa 2003 na baada ya miaka miwili baadaye mwaka wa 2005 walipata mtoto wa kike na Februari 5, 2005 walipeana talaka.

Shubhangi ameonekana katika maonesho mbalimbali yakiwemo Kasautii Zindagii Kay, Kasturi, na Chidiya Ghar. Pia ni maarufu wa kucheza Angoori Bhabhi huko Bhabhiji Ghar Par Hain.

Related Articles

Back to top button