Muziki

Shakira adondoka jukwaani na kuendelea na shoo

CANADA: MWANAMUZIKI Kutoka Colombia Shakira Mebarak maarufu Shakira, ameteleza na kudondoka jukwaani akiwa anatumbuiza jukwaani lakini cha kufurrahisha ni kwamba aliinuka na kuendelea na shoo yake kana kwamba hakuna kitu kilitokea kwake.

Tukio la kuteleza na kudondoka kwa mwanamuziki huyo lilitokea Mei 20, 2025 lakini video yake imeanza kusambaa kupitia mtandao wa X hivi karibuni ikizua minong’ono lakini wengi wanaoitazama video hiyo nao wameishia kumpongeza mwanadada huyo kwa kumudu shoo yake kama hakuna kilichotokea.

Video inamuonesha Shakira akiteleza na kuanguka vibaya akiwa katika ziara yake ya ‘Las Mujeres Ya No Lloran’ katika Kituo cha Bell huko Montreal, Quebec huko Canada.

Mwimbaji huyo wa ‘Hips Don’t Lie’ ambapo mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 48 alikuwa akiigiza kwa nguvu lakini ghafla akapoteza usawa wake na kuteleza kwenye jukwaa lakini alipoinuka kwa haraka mashabiki wake wakampigia makofi wakifurahia na kumpongeza kwa kuendelea na na onesho hilo kwa haraka.

Related Articles

Back to top button