Mastaa

Shah Rukh Khan: Silagi vyakula vya kifahari

MUMBAI: MUIGIZAJI Shah Rukh Khan mwenye miaka 59, ameweka wazi siri inayomfanya aonekane bado ananguvu kuliko waigizaji aliowazidi umri.

Amesema siri yake kuwa ni milo miwili kwa kila siku na huwa hanywi chai lakini pia.

Muigizaji huyo, ambaye hivi karibuni alitangaza kuacha kuvuta sigara amefichua. “Kwa kawaida mimi huegemea chakula cha msingi sana. Mimi hufuata milo miwili mikuu kila siku, chakula cha mchana na cha jioni. Kando na hivi, silagi vitafunio au kula kitu kingine chochote. Sipendi vyakula vya kifahari au vya hali ya juu. Milo yangu kwa kawaida sikula kuku wa kukaanga, wa mayai kwa miaka mingi.”

Walakini, mwigizaji huyo amesema “Ikiwa ninasafiri kwa ndege, au nyumbani kwa mtu kwa ajili ya chakula, nina chochote wanachotoa kwa neema iwe biryani, roti, parathas, chakula kilichopikwa na samli, au glasi ya lasi. Sijizuii wakati wa kushiriki mlo na wengine,” aliongeza.

Muigizaji huyo anaendelea kufichua siri zake kuwa pia halala kwa zaidi ya saa 5 kwa siku, na muda mwingi asubuhi huwa analala zaidi. “Kwa kawaida mimi hulala kitandani karibu saa 5.

Ameendelea kueleza kuwa kipindi cha kushoot kama muigizaji Mark Wahlberg anapoamka kuanza siku yake, Shah Rukh Khan anafunga siku yake. “Siku za kushoot, mimi huamka saa 9 au 10 asubuhi. Baada ya kurudi nyumbani usiku sana wakati mwingine saa mbili huoga na kupata mazoezi kabla ya kulala,” aliongeza.

Pia aliongeza kuwa amefanya kazi kwa bidii juu yake mwenyewe, “Nikiwa na umri wa miaka 55, niliamua kuchukua mapumziko yasiyo rasmi. Nakila mtu nilimwambia achukue likizo kwa ajili ya kujipanga upya, nilianza kujifunza vitu vipya na kufanya mazoezi. Nilijishauri mwenyewe, nilifanya kazi mara kwa mara, na kujenga mwili huu ninaojivunia sasa.”

Related Articles

Back to top button