Mastaa

Shah Rukh Khan, Priyanka Chopra, walaani shambulio la kigaidi la Pahalgam

KASHMIR: WASANII wa filamu Shah Rukh Khan, Alia Bhatt, Priyanka Chopra, Samantha Ruth Prabhu, Ibrahim Ali Khan, Karan Johar na wengine wengi wameonesha hasira yao baada ya shambulio la kigaidi huko Pahalgam, Jammu na Kashmir.

Takribani watu 26 waliuawa katika shambulio hilo lililozua wimbi la lawama kutoka kwa viongozi wa kisiasa na watu mashuhuri.

Mastaa hao na watu wengine mashuhuri kutoka tasnia ya burudani, wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kuelezea hasira zao baada ya shambulio hilo lililotokea hivi karibuni pamoja na kutoa rambirambi zao kwa shambulio hilo.

Wameeleza kuhuzunishwa kwao na shambulio hilo la kigaidi huku wakidai kilichotokea Pahalgam ni cha kulaumiwa.

Watu walikuwa likizo za kuvutia, wakisherehekea na familia zao wakiangaza uzuri wa Kashmir lakini walishuhudia maisha ya wapendwa wao yakimalizwa bila hatia.

Wamesema hili ni janga ambalo tunaweza kuondokana nalo. Shambulio hili baya linapaswa kutikisa dhamiri ya ubinadamu. Huku wakiamini jambo hilo litawatesa waombolezaji na waliohamishwa kwa muda mrefu hivyo kwa pamoja wanapaswa kuwaombea waliotangulia mbele za haki.

Wasanii hao wamesema, maisha ya watu wasio na hatia yamepotea. Watalii, familia, watu ambao walikuwa tu…. wakiishi. Kutafuta furaha na kuangalia uzuri wa Kashmir.

Hakuna chochote isipokuwa maumivu yanayotokana na vitendo vya uoga kama hivyo vya ugaidi. Hiki sicho ambacho Mungu wa mtu yeyote angekubali kamwe.

Related Articles

Back to top button