Sean ‘Diddy’ Combs kuhukumiwa Oktoba 3

NEWYORK: KESI ya mwanamuziki wa rap Sean Combs maarufu P Diddy ambaye wiki iliyopita aliachiliwa kwa ulanguzi wa ngono na ulaghai, lakini akapatikana na hatia ya makosa mawili ya usafirishaji kwenda kufanya ukahaba na sasa imethibitishwa kuwa atajua hatima yake katika muda usiozidi miezi mitatu.
Mawakili wa Diddy walipendekeza rasmi tarehe hiyo katika barua kwa Jaji Arun Subramanian, wakibainisha waendesha mashtaka na maafisa wa uangalizi walikuwa wamekubaliana na ratiba hiyo, gazeti la People linaripoti.
Mkataba wa hukumu wa timu ya utetezi lazima uwasilishwe Septemba 19, na ya serikali utafuatia wiki moja baadaye.
Mawakili wa pande zote mbili walifanya mkutano mfupi kwa njia ya simu jana mchana Julai 8, 2025, bila jaji au Diddy kuwepo.
Diddy alirejea katika Kituo cha Kizuizi cha Metropolitan huko Brooklyn mwishoni mwa kesi yake, huku hakimu akibainisha kuwa waendesha mashtaka walikuwa na haki ya kusema kwamba ukiukaji wa Sheria ya Mann unamaanisha kuwekwa kizuizini ni “lazima”.
Hakimu Subramanian amesema kuwa: “Kwa madhumuni ya sasa, mshtakiwa hawezi kukabiliana na mzigo wake na kabla ya kesi hiyo, mahakama ilikataa dhamana, na haioni sababu ya kutengua hilo kwa sasa.”
Na aliporudi gerezani, wakili wa Combs alidai alipokelewa kwa shangwe na wafungwa wenzake, ambao waliona hukumu hiyo kama ishara ya matumaini.
Combs alipatikana na hatia ya kusafirisha watu kuzunguka nchi nzima kushiriki ngono na anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 20 au zaidi jela.