Rais Samia aipongeza Yanga


RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Yanga kwa kufuzu hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ametoa pongoezi hizo kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.
“Kongole @YangaSC1935 kwa ushindi na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka la wanaume kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, msimu wa 2022/2023. Nawatakia kila la kheri katika hatua inayofuata,”amesema Rais Samia.
Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kuiondoa Club Africain ya Tunisia kwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano mjini Tunis Novemba 9.
Mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam Novemba 2 timu hizo zilitoka suluhu.
Yanga na Simba zinasubiri kujua zitapangwa makundi yapi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika wakati wa upangaji makundi hayo utakaofanyika Cairo, Misri Novemba 16.