Kwingineko
Samatta aikacha Fenerbahce

NAHODHA wa Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amejiunga na Klabu ya PAOK inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ugiriki.
Samatta amesaini kandarasi ya miaka miwili na timu hiyo na kipengele cha kuongeza mwingine mmoja zaidi.
Taaarifa zinaeleza kuwa Samatta amekamilisha dili hilo baada ya kuvunja mkataba na Fenerbahce ya Uturuki aliyojiunga nayo mwaka 2020 akitokea Aston Villa ya England.