EPL

Salah aweka rekodi PFA

MANCHESTER: Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA) mara tatu baada ya raia huyo wa Egypt kuchaguliwa tena hapo jana na kuhinda tuzo hiyo

Salah ambaye alijiunga na Liverpool mwaka 2017 alimaliza msimu uliopita kama mfungaji bora wa Premier League akiwa amefunga mabao 29 na asisti 18, akichangia pakubwa klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo, na kumaliza kwa pointi 10 mbele ya Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 tayari alikuwa ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Kiatu cha Dhahabu kwa mabao mengi zaidi na tuzo ya Playmaker kwa kutoa pasi nyingi za mabao na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo zote tatu kwa msimu mmoja.

Salah alishinda tuzo ya PFA kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018 baada ya msimu wake wa kwanza Liverpool kisha 2022, na mwaka huu akiibuka kidedea juu ya orodha ya wachezaji sita wa mwisho iliyopigiwa kura na wanachama wa PFA kutoka timu 92 za Ligi Kuu na Ligi nyingine za England.

Orodha hiyo ilijumuisha mchezaji mwenzake wa Liverpool Alexis Mac Allister, pamoja na Alexander Isak wa Newcastle United, Bruno Fernandes wa Manchester United, Declan Rice wa Arsenal na Cole Palmer wa Chelsea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button