Featured
‘Robertinho’ Kocha Mkuu Simba

KLABU ya Simba imemtambulisha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.
Kocha huyo ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Simba ametembulishwa leo katika mkutano wa viongozi wa Simba na waandishi wa habari, Dar es Salaam.
Kabla ya kujiunga na Simba ‘Robertinho’ alikuwa akiifundisha Vipers ya Uganda.