Mastaa

Rammy Galis azungumzia siri ya kumficha mke wake

DAR ES SALAAM:MKALI wa filamu nchini, Rammy Galis ‘Rammy’, amefunguka sababu ya kuficha maisha yake ya kimapenzi tangu alipofunga ndoa na mkewe miezi 9 iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, akisherehekea kumbukizi ya miezi 9 ya ndoa, msanii huyo aliandika:

“Si kila kitu kinachong’aa hutakiwa kuonekana. Baadhi ya hazina hufichwa ili zidumu thamani yake.Ndio maana maisha yangu ya ndoa yanabaki kuwa utulivu wangu wa siri. Ninapomlinda, si kwa sababu naogopa dunia bali kwa sababu ninajua thamani ya kile nilichopewa na Mungu”.

Kauli hiyo imeonesha jinsi anavyompenda na kumthamini mke wake, akiamini kuwa kumficha mitandaoni ni njia ya kulinda thamani na heshima ya ndoa yao.

Kwa mtazamo wako, je, ni sawa kumposti mwenza wako kwenye mitandao ya kijamii au ni vyema kumweka mbali na macho ya umma?

Related Articles

Back to top button