Nyumbani

Rais Mwinyi awahamasisha Simba kwa ahadi ya dola 100,000

ZANZIBAR:KATIKA  hekaheka za kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuwatia moyo wachezaji wa Simba SC kwa ahadi tamu  zawadi ya Dola 100,000 (sawa na sh milioni 267) iwapo watatwaa ubingwa huo.

Akiwa katika kambi ya Simba usiku wa Jumamosi Mei 24, Rais Mwinyi alikutana na kikosi cha timu hiyo,  ambapo leo Jumapili Simba inatarajiwa kushuka dimba la New Amaan Complex kwa mchezo wa marudiano dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Dkt. Mwinyi amewatakia mchezo mwema na kuwaeleza umuhimu wa mchezo wa kesho kwa nchi na hivyo serikali inatoa ushirikiano wa kila namna kuhakikisha tunaibuka na ushindi mkubwa ambao utatuwezesha kushinda ubingwa wa kombe hilo.

Simba  wanaingia uwanjani wakiwa na jukumu za  kuhakikisha wanashinda kwa tofauti ya mabao zaidi ya 3-0, baada ya kupoteza 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Morocco wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button