Burudani

‘Producer’ wa Michael Jackson afariki dunia

NEW YORK: Mtayarishaji nguli wa muziki Quincy Jones ambaye ndiye aliyetayarisha albamu ya ‘Thriller’ ya marehemu Michael Jackson amefariki akiwa na miaka 91.

Mtayarishaji huyo pia amefanya kazi na Celine Dion, Frank Sinatra na Ray Charles

Quincy Jones pia ndiye aliyeandika pamoja na kutoa wimbo wa hisani ‘We Are The World’ amekuwa mtunzi aliyefanikiwa zaidi katika ala nyingi za filamu zilizotamba duniani kote
Wapendwa wa Quincy wamesema katika taarifa yao: “Usiku wa leo (jana), Novemba 03, 2024, ndugu yetu Quincy Jones amefariki.

“Ingawa hii ni hasara ya kushangaza kwa familia yetu, tunasherehekea maisha mazuri ambayo aliishi na tunajua kamwe hakutakuwa na mwingine kama yeye.”

Kazi ya mtayarishaji huyo ilidumu zaidi ya miaka 70 na ameshinda Tuzo 28 za Grammy kati ya 80.

Pamoja na ‘Thriller’, pia ametayarisha ‘Off the Wall’ na ‘Bad’ kwa Michael Jackson na vile vile rekodi za Aretha Franklin, Donna Summer, George Benson na Dizzy Gillespie pia ametayarisha yeye.

Quincy Jones amezaliwa March 14, 1933, huko Chicago. Mama yake anaitwa Sarah Jones, alikuwa akifanya kazi benki na baba yake Quincy Delight Jones alikuwa fundi seremala.

Baada ya kusoma muziki alihamia New York baada ya kuajiriwa na kiongozi wa bendi ya Jazba Lionel Hampton na tamasha moja la mapema likipiga tarumbeta kwa Elvis Presley kwa maonyesho ya kwanza ya TV ya The King.

Hatimaye Quincy alipata kazi kama mtayarishaji katika studio ya muziki ya Mercury na kuanza kutunga filamu pia na ndiye alikuwa Mwafrika wa kwanza kuteuliwa kwa Tuzo ya Wimbo Bora wa Asili katika Tuzo za Oscar za 1968 kwa wimbo wa ‘The Eyes of Love’ kutoka kwenye filamu ya ‘Banning’, ikiwa ni teuzi wake wa kwanza kati ya saba.

Related Articles

Back to top button