EPLKwingineko
Pope nje miezi 4
GOLIKIPA wa Newcastle United na England, Nick Pope anahitaji kufanyiwa upasuaji na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi minne.
Pope,31, alipata jeraha la bega alipookoa hatari golini mwake dakika za mwisho wakati wa mchezo timu yake ilipopata ushindi wa bao 1-0 Desemba 2 dhidi ya Manchester United.
“Tunamfikiria kwa sababu ni jeraha lingine la ajabu kwetu. Hakuna shaka anahitaji kufanyiwa upasuaji hivyo atakuwa nje kwa muda,” amesema Kocha wa Newcastle, Eddie Howe.
Pope, ambaye alijiunga na Newcastle Juni 2022 kwa kiasi cha ada kisichoelezwa, anakuwa miongoni mwa majeruhi kadhaa kwenye klabu hiyo wakiwemo mshambuliaji Callum Wilson, winga Harvey Barnes, viungo Jacob Murphy na Joe Willock na mabeki Sven Botman na Dan Burn.




