Polisi yajipanga kulipiza kisasi kwa Mbeya City

TIMU ya Polisi Tanzania imejipanga kulipiza kisasi katika mchezo ujao dhidi ya Mbeya City Ligi ya Championship utakaochezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mjini Babati kesho Ijumaa.
Ofisa Habari wa timu ya Polisi Tanzania Frank Lukwaro amesema alama tatu za mchezo huo ni muhimu ikiwemo kulipa kisasi cha kufungwa na Mbeya City katika mchezo wa duru la kwanza katika Uwanja wa Sokoine Mbeya hivyo wameupa umuhimu mkubwa.
Katika mchezo wa kwanza Polisi Tanzania ilifungwa mabao 4-0.
Amesema mpaka sasa kikosi hicho kipo vizuri na hakuna majeruhi hivyo kilichobaki ni kuhakikisha kila mchezaji anapambana kuhakikisha wanapata ushindi.
Lukwaro ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo mjini Babati kujitokeza kwa wingi ili kushirikiana kwa kuwa itakuwa siku ya mapumziko.