
HUKU ikiendelea kushika mkia nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Polisi Tanzania leo ina mtihani itakapokuwa mgeni wa KMC.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
KMC inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 16 wakati Polisi Tanzania ina pointi 9 baada ya michezo 16 pia.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Singida Big Stars ni mgeni wa Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Singida BS ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 16 wakati Mbeya City ni ya 9 ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 16 pia.