Kwingineko
Pogba abeba tuzo baada ya kipindi kigumu

DUBAI:KIUNGO wa Ufaransa Paul Pogba ametwaa tuzo ya ‘Best Comeback’ kwenye hafla ya Globe Soccer Awards 2025, baada ya kurejea tena uwanjani kufuatia kipindi kigumu nje ya soka.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Pogba alisema safari yake haikuwa rahisi hata kidogo, lakini ilimfundisha kutambua watu waliokuwa karibu naye kwa dhati wakati hakuwa tena kwenye mwanga wa umaarufu. Alisema tuzo hiyo ina maana kubwa sana kwake na kwa familia yake, hasa mke wake ambaye alimsaidia sana kipindi chote kigumu, pamoja na watoto wake waliompa tabasamu wakati mambo yalikuwa mazito.
Pogba pia alitoa shukrani kwa klabu ya AS Monaco kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kurejea, pamoja na wachezaji wenzake na mashabiki wote waliomtumia ujumbe wa faraja alipokuwa kwenye wakati mgumu. Kwa tuzo hii, Pogba ameweka alama mpya kwenye safari yake ya kurejea kwenye soka la juu baada ya misukosuko mingi.




