Muziki

Pipi Jojo aachana na Chief Godlove

DAR ES SALAAM: MENEJA na Mkurugenzi wa Chief Loot Music, Chief Godlove, ametangaza rasmi kuvunjwa kwa mkataba wa usimamizi kati ya lebo hiyo na msanii Pipi Jojo, hatua inayomfanya msanii huyo kuwa huru kuanzia leo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chief Godlove ameweka wazi kuwa makubaliano ya kusimamia kazi za Pipi Jojo yamefikia tamati rasmi kuanzia Februari 24, 2026.

Katika taarifa hiyo, uongozi wa Chief Loot Music ulieleza:
“Uongozi wa Chief Loot Music kupitia Mkurugenzi wake Chiefgodlove billionaire, unapenda kuujulisha umma na wadau wa sanaa kuwa kuanzia leo Februari, 24, 2026 rasmi umemaliza makubaliano ya kumsimamia msanii Pipi Jojo.

“Hivyo basi, kuanzia tarehe hiyo, msanii huyu ni msanii huru na hayupo tena chini ya usimamizi wa lebo hii ya Chief Loot Music.

“Uongozi unatoa shukrani kwa ushirikiano uliokuwepo na unaomba wadau na mashabiki kuendelea kumpa sapoti katika hatua zake zinazofuata.

Imetolewa na Uongozi, Chief Loot Music.”
Hatua hiyo inafungua ukurasa mpya kwa Pipi Jojo, ambaye sasa atakuwa akisimamia kazi zake kama msanii huru.

Hata hivyo, haijawekwa wazi sababu za kuvunjwa kwa makubaliano hayo.

Wadau wa muziki na mashabiki wake sasa wanasubiri kuona mwelekeo mpya wa safari yake ya kisanii baada ya kuondoka chini ya usimamizi wa Chief Loot Music.

Spoti leo tumemtafuta Pipi Jojo aweze kuongeleea hilo hakupokea simu, bado tunaendelea kumtafuta atuambie nini sababu.

Related Articles

Back to top button