Phina: Nilianza kuimba kanisani

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Saraphina Michael ‘Phina’ amesema kuwa kipaji chake kilianza kuonekana kanisani hadi kuwafikia Watanzania na Dunia.
Amewataka watoto wa kike na mabinti kutokatishwa tamaa na kuzidi kupambania ndoto zao kwani ni marufuku kukata tamaa.
“Nimejifunza kwamba kama mtoto wa kike unapaswa kuishi ndoto zako na kutokata tamaa kwa aina yoyote. Unachopaswa wewe ni kupambania ndoto yako uliyonayo. Nilianza kuimba Kanisani, baadae nikawa naimba imba shuleni. Nilipomaliza nilienda Chuo na sikukata tamaa nikawa naenda kuomba kuimba Karioki iliyopelekea kuingia katika Shindano la kusaka Vipaji la Bongo Star Search na kuibuka mshindi ndipo watu wakazidi kunijua”, alisema Phina.
Pia amesema wimbo wa ‘Sisi ni wale’ aliuimba akihusianisha na ukweli wa maisha yake aliyopitia.