Partey afunguliwa mashtaka ya ubakaji

LONDON, Kiungo wa Kimataifa wa Ghana,Thomas Partey ameshtakiwa kwa makosa matano ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono aliyoyatenda kwa wanawake watatu tofauti.
Kwa mujibu wa mamlaka za kipolisi za jiji la London Partey alitenda makosa hayo jijini London na sehemu nyingine za nchi ya England na yanaripotiwa kutokea kati ya 2021 hadi 2022.
“Ofisi ya Waendesha Mashtaka wa kifalme imeidhinisha maombi ya mamlaka ya kipolisi ya London kumshtaki mtu mwanaume baada ya faili la ushahidi kuwasilishwa na wapelelezi”.
“Mamlaka ya kipolisi ilikua imetoa ombi na shtaka kwa Thomas Partey mwenye miaka 32 (13/06/1992), wa Hertfordshire, kuhusiana na makosa yafuatayo: Makosa matano ya ubakaji, na moja ya unyanyasaji wa ngono.” imesema taarifa ya Waendesha mashtaka
Mashtaka hayo yanawahusisha wanawake watatu wenye makosa mawili ya ubakaji yanayohusiana na mwanamke mmoja, makosa matatu ya ubakaji kuhusiana na mwanamke wa pili na moja la unyanyasaji wa kijinsia likihusishwa na mwanamke wa tatu.