Nyumbani

Pamba mali ya jiji la Mwanza

MKOA wa Mwanza umeikabidhi klabu ya Pamba kwa Halmashauri ya jiji hilo ili kuiendesha timu hiyo kwa uhakika wa bajeti.

Taarifa ya uongozi wa klabu ya Pamba iliyotolewa leo imesema shughuli zote za klabu kuanzia usajaili wa wachezaji, kambi na majukumu mengine yatafanywa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia Halmashauri ya jiji la Mwanza huku makabidhiano rasmi yakiendelea kufanyika.

“Kwa mantiki hiyo, Pamba Fc kuanzia sasa itaendeshwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza bila kuathiri jina lake la Pamba Football Club kwa kuwa timu hii ni nembo ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,”imesema taarifa hiyo.

Pamba iliyoanzishwa mwaka 1968 ilikuwa ikiendeshwa na wadau waliopewa timu hiyo na Ofisi ya Mkoa wa Mwanza baada ya klabu hiyo kutolewa na Mamlaka ya Pamba mwaka 1999.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button