EPL

Nuno yupo Forest hadi 2028

NOTTINGHAM, Meneja wa Nottingham forest Nuno Espirito Santo ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu zaidi hadi msimu wa joto wa 2028 baada ya kuisaidia klabu hiyo kufuzu kwa mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1995/96.

Nuno raia wa Ureno ambaye hapo awali alipita katika klabu za Wolverhampton Wanderers na Tottenham Hotspur, alijiunga na Forest mwezi Desemba 2023 na kusaidia timu hiyo kuepuka kushushwa daraja kabla ya kuiongoza kumaliza katika nafasi ya saba 2024-25, kampeni yao ya ligi bora zaidi ndani miongo mitatu.

Forest walikosa nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya walipomaliza kwa pointi moja nyuma ya Newcastle United waliomaliza katika nafasi ya tano, wakiangukia hatua ya playoff ya Conference League.

“Nina furaha kuweza kuendelea na safari yetu na katika klabu hii nzuri ya kandanda, Tumejitahidi sana kujenga uhusiano maalum kati ya wachezaji, mashabiki na kila mtu kwenye klabu, jambo ambalo lilitusaidia kufikia mafanikio makubwa msimu uliopita. Sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii zaidi kuliko wakati mwingine wowote tunapojitahidi kupata kumbukumbu maalum zaidi pamoja” – Nuno alisema

Related Articles

Back to top button