EPL

Nkunku hatihati kurejea msimu huu

KOCHA wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema hana uhakika kama mshambuliaji Christopher Nkunku atacheza tena msimu huu.

“Kwa sasa hafanyi mazoezi nasi …Anapata nafuu na inachukua muda mrefu kuliko tulivyotarajia”. “Tunatumai anaweza kuhusika tena haraka iwezekanavyo,” amesema Pochettino.

Nyota huyo raia wa Ufaransa amekuwa akikumbwa na majeraha tangu kuwasili kwake msimu 2023 akitoka RB Leipzig ya Ujerumani.

Mechi yake ya mwisho kama mchezaji wa akiba ilikuwa katika fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool mwezi Februari.

Jeraha la goti alilolipata wakati wa mechi ya kujiandaa na msimu uliopita wa kiangazi lilihitaji kufanyiwa upasuaji na kumweka nje kwa miezi minne ya kwanza ya msimu huku jeraha la nyonga lilimfanya akosekane kwa muda mwingi wa Januari.

Amecheza mechi 10 pekee katika mashindano yote msimu huu, nyingi kati ya hizo zikiwa kama mchezaji wa akiba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button