Mapinduzi CupNyumbani
Yanga au Singida BS kutinga nusu fainali Mapinduzi?

TIMU mbili zitakazoungana na Azam na Mlandege katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi zitajulikana leo.
Yanga na Singida Big Stars zitakutana kuhitimisha hatua ya makundi kutoa mshindi mmoja huku zote mbili zikiwa na pointi 3 baada ya kushinda michezo ya awali.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Namungo na Aigle Noir ambao utachezwa mapema kwenye uwanja wa amani.
Timu hizo zina pointi moja kila moja baada ya Aigle kutoka sare ya 1-1 na Chipukizi wakati Namungo imetoka suluhu na Chipukizi.