World Cup

Ni vita robo fainali Kombe la Dunia

VITA ya kufuzu nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inaendelea leo Doha, Qatar kwa michezo miwili ya mwisho katika hatua hiyo.

Katika mchezo wa kwanza miamba ya Afrika, Morocco itaikabili Ureno kwenye uwanja wa Al Thumama.

Mchezo wa pili utashuhudia England ikiivaa bingwa mtetezi Ufaransa kwenye uwanja wa Al Bayt.

Mshindi wa mchezo wa kwanza atapambana na mshindi wa mchezo wa pili katika nusu fainali.

Miamba ya Amerika ya Kusini, Argentina itakutana na Croatia katika nusu fainali baada ya timu hizo kuzitoa kwa njia ya penalti Uholanzi na Brazil Desemba 9.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button