Kwingineko
Ni PSG au Dortmund kutinga fainali UCL?

MCHEZO wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) kati ya Paris Saint-Germain na Borussia Dortmund unapigwa leo kwenye uwanja wa
Parc des Princes jijini Paris, Ufaransa.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ujerumani Mei Mosi, Dortmund ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya PSG.
Mshindi wa jumla wa mechi hiyo atakutana fainali na mshindi wa jumla kati ya Bayern Munich na Real Madrid ambazo zilitoka sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kwanza Aprili 30.