Ligi KuuNyumbani

Ni patashika Mbeya City vs Simba

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili Mbeya na Singida.

Wekundu wa Msimbazi, Simba ni wageni wa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Simba inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 27 baada ya michezo 12 wakati Mbeya City ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 12.

Katika mechi ya mwisho Mbeya City na Simba kukutana ligi kuu Julai 3, 2022 msimu wa 2021/22 Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga kwa mabao 4-1, Singida Big Stars itakuwa uwanja wa nyumbani Liti mjini Sinigda kuivaa KMC.

Singida BS ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 11 wakati KMC inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 12.

Novemba 22 imefanyika mechi moja ya ligi kwenye uwanja wa Liti mkoani Singida ambapo Yanga imeiibuka washindi dhidi ya Dodoma Jiji kwa mabao 2-0.

Yanga sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 29 sawa na Azam lakini ina mabao mengi ya kufunga huku Dodoma jiji ikiwa nafasi ya 15 ikijikusanyia pointi 9 baada ya michezo 12.

Related Articles

Back to top button