Kwingineko
Ni nusu fainali ya kisasi El Clásico

MCHEZO wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Hispania inapigwa leo kwa mtanange wa El Clásico kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Santiago Bernabeu ukiamuliwa na mwamuzi wa kati
Jose Munuera.
Kwa Barcelona utakuwa ni mchezo wa kisasi baada ya kufungwa magoli 3-1 na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania(Laliga) Oktoba 16, 2022.
Real Madrid itataka kulipiza kisasi baada ya kuchapwa magoli 3-1 na Barcelona katika fainali ya Super Cup iliyopigwa Riyadh, Saudi Arabia Januari 15, 2023
Nusu fainali ya pili kombe la mfalme itakuwa Athletic Bilbao dhidi ya Osasuna.