EuropaKwingineko
Ni kisasi Barca vs Man U Europa

MICHEZO nane ya kwanza ya raundi ya mtoano michuano ya Ligi ya Europa inapigwa leo huku kipute kati ya Barcelona na Manchester United kikiwa kivutio.
Michezo kati ya timu hizo kila zinapokutana huvutia hisia za mashabiki wengi kutokana na hadhi za timu hizo.
Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika miaka ya hivi karibu kati ya timu hizo yanaonesha Barcelona ikipata ushindi mara nyingi zaidi kuliko Manchester United.
Michezo mingine ya Europa leo ni kama ifuatavyo:
Ajax vs Union Berlin
FC Salzburg vs Roma
Shakhtar Donestsk vs Rennes
Juventus vs Nantes
Sevilla vs PSV Eindhoven
Sporting CP vs FC Midtjylland