Michezo MingineRiadha

Ngorongoro Half Marathon 2022: Ni mbio inayosapoti Royal Tour

MSIMU wa 14 wa Ngorongoro Marathon 2022 umepangwa kufanyika Septemba 11 na kushirikisha wanariadha kibao wa ndani na nje ya nchi.

Mbio hiyo ya kila mwaka imekuwa na mafanikio makubwa, huku mwaka huu kauli mbiu ikiwa ni kuunga mkono mikakati ya Rais Samia Hassan Suluhu ya kuhamasisha watalii kutembelea Tanzania.

Samia hivi karibuni alizindua filamu ya Royal Tour nchini Marekani kabla ya kufanya hivyo Arusha, Zanzibar, Dar es Salaam na kwingineko ili kuhamasisha watalii kutembelea vituo nchini.

MBIO ZENYEWE

Ngorongoro Half Marathon 2022 imekuwa ikianzia katika lango la kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na kumalizikia katia viwanja vya michezo vya Mazingira Bora vilivyopo mjini Karatu, ambako zawadi hutolewa kwa washindi.

Wakati mbio ya kilometa 21 imekuwa ikianzia katika lango la Ngorongoro, zile za kilometa 10 na 5 zenyewe zitaanzia na kumalizikia kwenye Uwanja wa Mazingira Bora.

Mbio hizo zimekuwa zikiwashirikisha wanariadha nyota kutoka ndani nan je ya nchi kutokana na mazingira zinapoanzia huko Ngorongoro, ambako kuna vivutio vikubwa vya utalii, likiwemo bonde la Ngorongoro.

Baadhi ya wanariadha nyota ambao wamekuwa wakishiriki mara kwa mara mbio hizo ni pamoja na bingwa wa medali ya fedha ya Jumuiya ya Madola, Alphonce Simbu, Failuna Abdi, Sarah Ramadhani, Emmanuel Giniki, Jackline Sakilu na wengine.

MAANDALIZI

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mbio hiyo Meta Petro, tayari usajili umeanza na utaendelea hadi siku moja kabla ya kufanyika kwake, Septemba 10. Meta anasema kuwa wale wanaotaka kushiriki mbio hizo wanatakiwa kujisajili kupitia namba ya simu +255- 754 821 380 au kwa kutumia lipa namba 5386444 gharama ya kushiriki ni Sh 35.000 kwa mtu.

Anasema kuwa maandalizi yana kwenda vizuri kwa ujumla na wanariadha wameshaanza kujiandikisha wakiwahi namba kwani mwaka huu wanatarajia kuwa na washiriki wengi kutokana na ubora wa mbio hiyo.

Meta ambaye ni mwanariadha wazamani wa kimataifa wa Tanzania anasema kuwa mwaka huu ada ya ushiriki ni moja tu kwa mbio zote, yaani za kilometa 21, 10 na tano za kujifurahisha.

WADHAMINI

Meta anasema kuwa tayari Kampuni ya Bonite Bottlers imeshathibitisha kuwa mingoni mwa wadhamini wa mbio hizo huku wakitarajia wengine kujitokeza wakati wowote kufanikisha mbio hiyo.

Anasema kuwa milango iko wazi kwa ajili ya wadhamini mbalimbali kujitokeza kwani itawasaidia kutangaza bidhaa au huduma zao kupitia mbio hiyo.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imekuwa ikidhamini mbio hiyo kila mwaka na mwaka huu imeonesha nia ya kufanya hivyo, lakini inakamilisha baadhi ya vitu kabla ya kutangaza rasmi udhamini huo.

Meta anasema kuwea NCAA ni wadau wakubwa wa mbio hiyo na riadha kwa ujumla, hivyo ni mataumaini yao kubwa mwaka huu wataendelea kuwa sehemu yam bio hiyo.

ZAWADI NONO

Waandaaji wa Ngorongoro Half Marathon 2022 wanasema kuwa hivi karibuni watatangaza zawadi nono kwa ajili ya washindi wa mwaka huu, na kuwataka wadau kukaa mkao wa kula wakisubiri.

KUIBUA VIPAJI

Pamoja na mengi yote ya kusaidia jamii na mengine, mbio hiyo imekuwa na lengo la kuibua na kuinua vipaji vya wanariadha chipukizi na kuwawezesha kutumia riadha kama ajira yao ya kudumu.

Meya anasema kuwa wamekuwa wakiwasaidia vijana kuibua vipaji vyao na hata kuviendeleza na kuwafanya kuwa wanariadha wakubwa huko mbele, ambao watatumia riadha kuwa ajira yao ya kudumu.

Amewataka washiriki kujitokeza kwa wingi katika mbio za kilometa 21, ambazo huwa na ushindani wa hali ya juu na zile za kilometa 10 pamoja na kilometa 5 za kujifurahisha.

Related Articles

Back to top button