Featured
Neymar ateguka kifundo cha mguu

KLABU ya Paris Saint-Germain imethitbisha kwamba mchezaji wake Neymar Jr amepata majeraha ya kuteguka kifundo cha mguu.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil aliondolewa uwanjani kwa machela dakika 30 tu tangu kuanza mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa kati ya timu yake na Lille Februari 19 PSG ikishinda kwa magoli 4-3.
“Uchunguzi mpya umethibitisha kuwa Neymar Jr aliteguka kifundo cha mguu. Vipimo zaidi vitafanyika mwanzoni mwa wiki ijayo,” imesema taarifa ya PSG.
Neymar ataukosa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake na Bayern Munich utakaopigwa Machi 8.