EPL

“Newcastle nisubirini” – Howe

NEWCASTLE: MENEJA wa Newcastle Eddie Howe amethibitisha kuwa hayuko fiti kwa asilimia mia moja kurejea katika kazi ya kuendelea kuinoa Newcastle msimu huu baada ya kocha huyo kuugua maradhi ya pneumonia yaliyomuweka hospitalini tangu mapema mwezi huu.

Howe alilazwa hospitali baada ya kutojisikia vizuri kwa siku kadhaa, akiikosa michezo kadhaa ya klabu yake ikiwemo ile ya Manchester United, Crystal Palace, na Aston Villa baada ya mapema msimu huu kuiongoza timu hiyo kutwaa taji lake la kwanza baada ya miaka 56 na sasa bado hayuko tayari kurejea kazini.

“Niko sawa, japo sio kwa asilimia 100 kimwili lakini nadhani niko karibu na kuwa sawa kichwani kwangu jambo ambalo ndio la muhimu sana. Nimepitia mengi sana kipindi hiki lakini nashukuru niko kwenye njia sahihi inayonielekeza kwenye kupona ni jambo muhimu na bora zaidi na ninafurahi kuwa hapa” Eddie Howe amewaambia wanahabari

“Ni vyema kujisikia hivi lakini kujua mashabiki wanataka kuniona tena kazini inanifariji nawaambia niko njiani wanisubiri” aliongeza

Tangu kuugua kwa kocha huyo mwenye miaka 47 Newcastle imekuwa chini ya kocha msaidizi Jason Tindall ambaye ameisaidia klabu hiyo kushinda michezo muhimu ukiwemo ule dhidi ya Manchester United huku akipokea kichapo cha 4-1 kutoka kwa Aston Villa.

Newcastle walio nafasi ya 5 kwenye msimamo wa Ligi wakiendelea kupambania nafasi katika Ligi Ya Mabingwa msimu ujao watakuwa na meneja wao Eddie Howe wikiendi hii watakaowakaribisha St James’ Park Ipswich walio katika hatari ya kurudi Championship msimu ujao.

Related Articles

Back to top button