Ligi KuuNyumbani

Namungo kusajili, kuacha wachezaji

KOCHA Mkuu wa Namungo Denis Kitambi amesema klabu hiyo inapanga kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji wanne wapya kwenye dirisha dogo.

Akizungumza na SpotiLeo kocha huyo amesema mbali na kusajili wanne pia Namungo itaachana na baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka viwango.

“Namungo tuna malengo yetu ndio maana tumeshtuka baada ya kuona mzunguko wa kwanza hatujafanya vizuri kama tulivyotarajia,” amesema Kitambi.

Kitambi ambaye amempokea Honour Janza raia wa Zambia katika nafasi hiyo amesema kklabu hiyo itasajili washambuliaji wawili, kiungo mmoja na beki wa pembeni mmoja.

Namungo yenye makao yake Ruwangwa mkoani Lindi inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikikusanya pointi 18 katika michezo 15.

Related Articles

Back to top button