Nahodha: Kadi nyekundu ndiyo iliyotupa sare dhidi ya Angola

KENYA: NAHODHA wa Harambee Stars, Aboud Omar amesema kadi nyekundu aliyopewa kiungo wao Marvin Nabwire iliwapa wakati mgumu kupata alama tatu na badala yake wakapata alama moja ngumu dhidi ya Angola katika mchuano wao mgumu uliopigwa jana nchini Kenya.
Kenya ililazimika kujipanga kutoka nyuma baada ya Jo Paciencia kuwapa wageni bao la kwanza dakika ya saba, akimpita kipa na kuwanyamazisha mashabiki wa Kenya.
Hata hivyo, dakika tano tu baadaye, Austin Odhiambo alirejesha furaha kwa Wakenya baada ya kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati.
Aboud anasema hali ilikuwa ngumu baada ya Nabwire kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu kwenye eneo la hatari, na kuwalazimu Harambee Stars kucheza kwa zaidi ya dakika 70 na wachezaji kumi.
“Kadi nyekundu ya Marvin ilikuja kama kitendo cha ujasiri, alichukua moja kwa timu. Ilituhudhunisha lakini pia ilitutia moyo sababu kama angemruhusu mpinzani kumpiga chenga, basi tungepoteza mchezo,” Omar amesema.
Pia alisifu marekebisho ya kimbinu ya Kocha Bennie McCarthy ambayo yalisaidia timu hiyo kucheza kwa nidhamu mno kwa kufuata mipango yake.
“Wakati wa mapumziko, kocha alituambia tulichotakiwa kufanya tukiwa chini ya mtu mmoja, jinsi tutakavyocheza. Wachezaji pia waliongezeka. Kwa ubora kutoka kwa wapinzani, lazima ufanye mengi ya ziada,” aliongeza.
Sare hiyo inawaweka Kenya katika hali nzuri huku wakijiandaa kwa mchuano wao ujao