Habari Mpya

Nabi ajivunia kikosi chake

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kinaimarika siku hadi siku na hiyo ndio sababu kubwa ya kupata ushindi karika michezo ya timu hiyo.

Amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kupata pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Tulistahili kushinda kutokana na kiwango tulichonesha lakini pia tuliutawala mchezo kwa asilimia kubwa kitu kizuri kwangu hatukuruhusu bao,” amesema Nabi.

Kocha huyo ameeleza kuwa mwenendo huo unazidi kumpa matumaini ya kutetea mataji yao bayo wanayashikilia kwa sasa.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara Septemba 13, 2022.

Related Articles

Back to top button