Ligi KuuNyumbani

Mwisho wa zama za vijana wa kizazi kipya?

HEKAHEKA za kuitafuta timu moja iliyosalia kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao bado zinaendelea, vijana wa kizazi kipya Mbeya City wanaendelea kupitia mitihani ya kuitafuta tiketi ya ligi kuu msimu ujao ambapo leo watavaana na na Mashujaa ya Kigoma.

Mbeya City ambao watakumbukwa kwa ubora wao kwenye ligi kuu tangu walipopanda mwaka 2013 wanapumulia mashine kwani kama watashindwa kuisambaratisha Mashujaa basi itakuwa ndio mwisho wa simulizi za Mbeya City kwenye ligi kuu.

Mchezo wa leo utapigwa kwenye dimba la lake Tanganyika mkoani Kigoma kabla ya mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

 

Related Articles

Back to top button