Nyumbani
Mwili wa Mzee Samatta kuzikwa kesho

DAR ES SALAAM: MWILI wa Mzee Ali Pazi, baba mzazi wa nahodha wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, unatarajiwa kuzikwa kesho, Jumatatu Julai 7, kijijini kwao Kibiti, Rufiji.
Mtoto wa marehemu, Mohammed Samatta, amesema maandalizi ya safari ya mwisho ya mpendwa wao yanaaendelea ambapo mwili utaondoka nyumbani kwake Mbagala jijini Dar es Salaam asubuhi, kuelekea Rufiji kwa maziko.
“Mwili wa marehemu baba yetu, Mzee Ali Pazi, utasafirishwa kesho Jumatatu Julai 7, kwenda kuzikwa nyumbani kwao Kibiti, Rufiji,” alisema Mohammed.
Mzee Pazi alifariki dunia leo Jumapili, Julai 6, katika saa za asubuhi kutokana na changamoto za kiafya zilizokuwa zikimsumbua kwa muda mrefu.
Raha ya milele umpe Ee Mola, na mwanga wa milele umuangazie. Amina.