‘Mwamba’ Haaland analipwa bil 2.2/- kwa wiki

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Erling Haaland analipwa pauni zinazokaribia 900,000 sawa na shilingi bilini 2.35 kwa wiki, ripoti zimesema.
Nyota huyo wa kimataifa wa Norway amewasha moto Ligi Kuu ya Uingereza tangu asajiliwe City kwa pauni milioni 51 sawa na shilingi bilioni 133.2 kutoka Borussia Dortmund.
Anapokea kiasi hicho kikubwa kinachomfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Uingereza.
Kwa mujibu wa ripoti hizo kiasi kikubwa cha bonasi kinafanya Haaland mwenye umri wa miaka 22 apate mshahara unaofikia zaidi ya pauni 850,000 sawa na shilingi bilioni 2.2 kwa wiki.
Bonasi hizo za moja kwa moja zitamfanya Haaland alipwe pauni milioni 45 sawa na shilingi bilioni 117.5 kwa mwaka.
Tayari amefunga mabao 14 katika michezo 8 ya Ligi Kuu katika kiwango ambacho kuna uwezekano akamaliza ligi akiwa amefunga mabao 67.