Ligi Kuu

Mukwala aweka Hat-Trick, mbio za Ubingwa zakolea

ARUSHA: MSHAMBULIAJI wa Simba, Steven Mukwala, ameendelea kuonesha ubora wake baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mukwala alifungua karamu ya mabao katika dakika ya 30, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 47, na kukamilisha hat-trick yake dakika ya 56. Ushindi huu umeiwezesha Simba kuendelea vyema na kampeni yao ya kusaka pointi 30 muhimu katika duru la pili la Ligi kuu ya NBC.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 54, huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi huku wakijiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya vinara wa ligi, Yanga, ambao wana alama 58.

Related Articles

Back to top button