Filamu

Muigizaji mkongwe Rajesh afariki dunia huko Chennai

CHENNAI:MUIGIZAJI mkongwe na mfanyabiashara Rajesh Williams, ambaye ameigiza katika mamia ya filamu na vipindi vya televisheni vya Kitamil na Kimalayalam, amefariki dunia leo Mei 29 huko Chennai nchini India.

Rakesh amefariki akiwa na umri wa miaka 75. Kupitia kazi yake, Rajesh alijulikana kwa kucheza nafasi mbalimbali kama muigizaji mkuu na msanii msaidizi wa wahusika.

Mpwa wa Rajesh alithibitisha habari kwa DT Next kwamba muigizaji huyo amefariki jana Alhamisi. Alikuwa akilalamika kuumwa shinikizo la chini la damu lakini asubuhi ya leo Mei 29 amefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Ameacha binti Divya na mwanawe Deepak, ambaye alianza kama muigizaji mwaka wa 2014. Mkewe, Joan Sylvia Vanathirayar, naye amefariki mwaka wa 2012 hivyo watoto wao hawana baba wala mama.

Watoto wake wanaomboleza kifo cha baba yao huku wakiwa na mengi ya kukumbuka na kumuenzi. Apumzike kwa amani mkongwe wa filamu nchini India Rakech Williams.

Related Articles

Back to top button