Mahusiano

Muigizaji mkongwe atamani kuolewa tena

NIGERIA: MUIGIZAJI mkongwe wa Nollywood, Bukky Wright, ameeleza nia yake ya kuolewa tena licha ya umri wake wa miaka 58.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 58 alifahamisha hayo katika mahojiano yake na BBC Yoruba.

Huku akionesha nia yake ya kuwa na mpenzi mpya, Bukky Wright amesisitiza kwamba nia yake ya kuolewa tena ipo pale pale.

“Kuhusu suala la ndoa, natamani kuolewa tena kama Mungu ameamua, lakini sio lazima.

“Kwa kweli, nilipoenda Al Kaaba niliomba kwa Mungu kuhusu hilo na ninajua yeye ni Mungu anayejibu maombi,” ameeleza.

DAILY POST limeripoti kuwa mama huyo wa watoto wawili alijipatia umaarufu mwaka wa 1999 kufuatia uhusika wake katika filamu ya ‘Saworoide’.

Related Articles

Back to top button