Msimu mpya wa soka DStv wa moto!

DAR ES SALAAM: Msimu mpya wa soka wa 2025/2026 umefika, na kauli mbiu ni moja tu – “It’s On!” Moto wa kandanda kutoka ligi kubwa duniani sasa unawaka rasmi kupitia SuperSport ndani ya DSTV – jumba halisi la soka.
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa msimu huu uliofanyika leo Julai 15 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa DSTV Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema msimu huu utakuwa wa aina yake huku mashabiki wakijipanga kushuhudia mechi kali, magoli ya kusisimua na burudani isiyo na kifani.
“Ni patashika nguo kuchanika. SuperSport iko tayari kuwapa wateja wa DSTV uhondo wa michuano mikubwa duniani, ikiwemo Premier League, Serie A, La Liga, michuano ya CAF kama CHAN, AFCON, CAF Champions League na nyinginezo,” amesema Shelukindo.
Shelukindo amewataka wateja wa DSTV kuhakikisha wanalipia visimbuzi vyao mapema au kujiunga upya ili wasikose tamasha hili la kandanda ambalo litaanza rasmi Agosti 10 kwa mechi ya FA Community Shield baina ya Liverpool na Crystal Palace.
Katika msimu uliopita, Liverpool walirejesha taji la EPL, Napoli wakanyakua Serie A na Barcelona wakiwazidi kete Real Madrid na kuchukua ubingwa wa La Liga chini ya kocha mpya Hansi Flick. Msimu huu, swali kubwa ni: Je, watatetea mataji yao?
Burudani itaendelea na mechi kali kama UEFA Supercup kati ya PSG na Tottenham Agosti 13, huku Napoli wakifungua kampeni yao ya Serie A dhidi ya Sassuolo mnamo Agosti 23.
Kwa mujibu wa DSTV, mashabiki wanaweza kufuatilia mechi zote mubashara kupitia SuperSport, iwe kwenye runinga, DSTV Stream au vifaa vya kidijitali kama simu, laptop na tablet. Kwa msimu huu, hakuna anayepaswa kukosa.
“Burudani hii ni ya wote, popote ulipo. Msimu huu wa 2025/2026 ni zaidi ya soka – ni sherehe ya mabingwa duniani kupitia SuperSport,” amesema
Katika hatua nyingine watangazaji wa michezo hiyo ambao ni Nazareth Upete, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ Ahmed Abdallah, Edgar Kibwana na Geofrey Lea wamesema msimu huu wamekuja kivingine.