Tetesi

Mshahara wa Benzema uarabuni kufuru

MKATABA wa Karim Benzema kunako Al Ittihad utamfanya apokee Euro milioni 200 (€200m) ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 500 kwa mwaka.

Mkataba wa Benzema utaisha Juni 2025 ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja, kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano.

Romano amesema mkabata umeshasainiwa na muda wowote kuanzia sasa klabu hiyo itatoa taarifa rasmi.

Mfaransa huyo anatarajiwa kutambulishwa mara baada ya taarifa ya Al Ittihad.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button